Viongozi wa kijadi wamtaka Gadafi kuachia ngazi

Viongozi wa Kijadi nchini Libya wamemtaka Kiongozi wa Taifa hilo Kanali Muammar Gaddafi kuachia madaraka wakati huu ambapo Waasi wakishirikiana na Majeshi ya NATO wakifanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikali. 

Matangazo ya kibiashara

Machief na Wawkilishi wa Makabili wapatoo sitini na moja wametangaza msimamo wao wa kutaka kanali Gaddafi aondoke madarakani kutokana na kushuhudia nchi hiyo ikiwa kwenye umwagikaji mkubwa wa damu.

Kauli ya Viongozi hawa wa kijadi inakuja wakati mashambulizi yanazidi kuchacha katika Mji wa Misurata ambayo ndiyo ngome ya Waasi huku taarifa zikisema majeshi ya Kanali Gaddafi yameshambulia bandari iliyopo kwenye mji huo.

Wakati mashambulizi yakizidi kushika kasi Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Liam Fox amekiri kuridhishwa na hatua ya Marekani kutoa ndege zake na kufanya mashambulizi kuwasaidia Waasi.

 

Katika hatua nyingine Serikali ya Libya imeendelea kusisitiza hatua ya majeshi yake kusitisha operesheni zake katika Mji wa Misurata licha ya uwepo wa taarifa za wao kuwepo kama anavyoeleza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Abdul Latif Al Obeidi.

Hakika hamkani si shwari nchini Libya kutokana na kuendelea kuwepo kwa idadi kubwa ya vifo kwenye nchi hiyo huku wakazi wa Misurata wakiwa katika uhitaji mkubwa wa msaada wa kibinadamu.