Libya

Umoja wa Mataifa UN waondoa wafanyakazi wake nchini Libya

Ofisi za Italia, Marekani na Uingereza za shambuliwa na waandamanaji wafuasi wa Gadaffi
Ofisi za Italia, Marekani na Uingereza za shambuliwa na waandamanaji wafuasi wa Gadaffi Reuters/Louafi Larbi

Umoja wa Mataifa UN umewaondoa wafanyakazi wake nchini Libya kutokana na hali ya machafuko kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, amesema kuwa hatua hiyo ni katika kukabiliana na watu wenye hasira kuingia kwenye eneo la umoja huo pamoja na kushambulia balozi za Uingereza na Italia mjini Tripoli.
Balozi hizo zilishambuliwa jana Jumapili kutokana na kuuawa kwa mtoto wa kiume wa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, Saif al-Arab. Kutokana na mashambulio hayo, Uingereza imemfukuza balozi wa Libya aliyeko mjini London na kumpa muda wa saa 24 kuondoka nchini humo.
Aidha, Askofu wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Tripoli, Mhashamu Giovanni Martinelli, amethibitisha kuhusu kifo cha Saif al-Arab, wakati akihojiwa na televisheni ya Italia. Askofu Martinelli ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa kuhusu uvamizi wa kijeshi wa mataifa ya Magharibi nchini Libya, pia ametaka kusitishwa kwa mapigano nchini humo.