RWANDA

Ufaransa yapandwa na hasira kutokana na matamshi ya Rais Kagame

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame REUTERS/Finbarr O'Reilly

Ufaransa imepandwa na hasira kutokana na matamshi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame dhidi ya Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ufaransa Alain Juppe katika gazeti la Jeune Afrique.

Matangazo ya kibiashara

Katika ukurasa mojawapo wa gazeti hilo, Rais Kagame amesema Alain Juppe hastahili kupokelewa nchini Rwanda na wala sio mtu mwenye umuhimu wowote. Wakati huohuo waziri huyo wa Ufaransa katika mkutano na vyombo vya habari alijibu na kusema kwamba hana nia ya kuelekea Rwanda na wala dhamira ya kumpa Kagame mkono. Alain Juppe alikuwa waziri wa mambo ya kigeni mwaka 1994 wakati yalipotokea mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Uhusiano kati ya Rais Kagame na waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Alain Juppe unazidi kuzorota licha ya juhudu za kuleta muafaka baina ya Rwanda na Ufaransa baada ya Rwanda kuishutumu Ufaransa kuhusika kwa njia moja ama nyinginde katika kuwasaidia watu waliosadikiwa ndiowalioendesha mauaji ya kimbari.

Wakati wa uteuzi wake kwenye uadhifa huo, Rais Kagame alisema kuwa Rwanda imetukanwa na kurefusha ziara yake ya kwanza rasmi nchini Ufaransa hadi Julay mwaka 2011

kwa sasa ni kupitia gazeti hilo la Jeune Afrique ndipo Rais Kagame adhihirisha hasira yake dhidi ya waziri huyo wa Ufaransa.

Mwaka 1994 Alain Juppe akiwa kwenye uadhifa huo alishutumiwa kuhusika pamoja na viongozi wengine 12 wa Ufaransa kuhusika katika kumsaidia rais wa Rwanda wa zama hizo Juvenal Habyarimana. Alain Juppe amekuwa akitetea siasa ya Ufaransa hasa pale Bernard Kuchner aliposema ni kosa kubwa la kisiasa la Ufaransa wakati wa mauaji ya kimbari.