Wapinzani nchini Burundi wapinga sheria ya kuorodhesha vyama upya

Ramani ya Burundi
Imehaririwa: 06/05/2011 - 12:02

Viongozi wa Vyama vya siasa nchini Burundi,vilivyosajiliwa kupitia mazungumzo ya Amani na mikataba vilioafikiana mjini Arusha nchini Tanzania baada ya kuweka chini silaha, vinasema havikubaliani na sheria mpya nchini humo ya kuvitaka kusajiliwa upya. Joseph Karumba ni kiongozi wa chama cha FROLINA, chama ambacho kimekuwa kikipambana na serikali kwa muda mrefu na amemueleza mwandishi wetu wa Bunjumbura Hassan Ruvakuki ni kwa nini hawataki chama chao kusajiliwa tena.