Abyei - Machafuko

Watu 14 wapoteza maisha mjini Abyei

Mji wa Abyei.
Mji wa Abyei. (Photo: Reuters)

Watu kumi na wanne wamepoteza maisha nchini Sudan kwenye Jimbo lenye Utajiri Mkubwa wa Mafuta la Abyei kufuatia kutokea mashambulizi punde tu baada ya msafara wa kijeshi ulikuwa umesheheni silaha za kivita kuvamia eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa ambazo zimethibitishwa na Kiongozi Mkuu wa eneo hilo Deng Arop Kuol zimeeleza magari sita yakiwa na wanajeshi zaidi ya mia mbili yalishuhudiwa yakivuka mpaka na kuingia Abyei.
Mashambulizi ambayo yamefanywa yamesababisha vifo kwa wanajeshi kutoka Jeshi la Sudan Kusini SPLA kitu ambacho kimechangia Uongozi wa eneo hilo kulaani vikali kile ambacho kimetokea.