GABON

Bunge la Gabon laondoa kinga kwa kiongozi aliyejitangaza Rais na kuunda serikali

Waziri mkuu wa zamani wa Gabon Eyéghé Ndong (Kweny Mic) pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya ndani, André Mba Obame, wakati wa mkutano na vyombo vya habari
Waziri mkuu wa zamani wa Gabon Eyéghé Ndong (Kweny Mic) pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya ndani, André Mba Obame, wakati wa mkutano na vyombo vya habari AFP

Wabunge nchini Gabon jana walipiga kura kuondoa kinga kwa kiongozi wa upinzani Andre Mba Obame ambaye alijitangaza mshindi wa uchaguzi wa Urais,na hatua hiyo imefungua njia ya kufunguliwa mashtaka kwa kiongozi huyo wa upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imekuja baaada ya waziri wa sheria wa Gabon Ida Assonouet kuwasilisha ombi la kuondolewa kwa kinga hiyo katika barua aliyomwandikia spika wa bunge la nchi hiyo March Kumi na nne mwaka huu.

Mba obame waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Gabon alijitangaza mshindi wa urais wa mwaka 2009 uliomweka madarakani rais Ali Bongo ,hatua iliyoelezewa na waziri wa sheria kuwa ilihatarisha mno usalama wa nchi hiyo.
Chama chake kilivunjwa tarehe 27 january mwaka huu.