CHAD

Kiongozi wa Upinzani nchini Chad afariki dunia kwenye kampeni

Jenerali Wadal Abdelkader Kamougue (Kulia) enzi za uwahi wake akiwa na Kiongozi wa Chama cha NURD Kebzabo Saleh (Kushoto)
Jenerali Wadal Abdelkader Kamougue (Kulia) enzi za uwahi wake akiwa na Kiongozi wa Chama cha NURD Kebzabo Saleh (Kushoto) AFP / Gaël Cogne

Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Chad ambaye pia anatajwa kuwa nguli wa kisiasa katika taifa hilo Jenerali Wadal Abdelkader Kamougue amefariki duniani akiwa na umri wa miaka 72.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa Chama Cha URD amekutwa na mauti akiwa katika kampeni ambapo alikuwa anamsaidia mkewe ambaye amekuwa akipambana kuhakikisha anashindwa uchaguzi wa Ubunge utakaofanyika siku ya ijumaa.

Vyanzo vya habari kutoka kambi ya Upinzani na Ofisi ya Rais Idriss Deby zimethibitisha kifo cha Jenerali Kamougue ambaye anatajwa kutaka kufanya majaribio ya kuangusha serikali mara nne wakati wa uhai wake.

Saleh Kebzabo ambaye ni Kiongozi wa NURD amesema Jenerali Kamougue alianguka kwenye mvua mapema asubuhi na taarifa zinaeleza tangu juma lililopita alikuwa mgonjwa.

Kifo chake kinakuja wakati ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi inajiandaa kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa Rais ambayo yalifanyika mwezi uliopita ambapo Kambi ya Upinzani ilisusia.

Mnamo tarehe 25 mwezi April Jenerali Kamougue aliitisha maandamano ya kupinga uchaguzi ambao ni wazi matokeo yake yatamrudisha Rais Deby madarakani kwa kipindi kingine.

Jenerali Kamougue alizaliwa Kusini mwa Gabon mnamo mwake 1939 ambapo Baba yake alikuwa Mwanajeshi wa Jeshi la Ufaransa ambapo naye aliamua kufuata kazi ya baba yake na alikuwepo kwenye Mapinduzi ya kumuangusha Rais wa kwanza wa Chad, Ngarata Tombalbaye mwaka 1975.