Afrika ya kati

Serikali yatangaza msiba wa kitaifa wa siku 7 nchini Afrika ya kati

Ange-Felix Patassé, mjini Bangui, Januari 23, 2011.
Ange-Felix Patassé, mjini Bangui, Januari 23, 2011. AFP / PATRICK FORT

Mwili wa hayati Ange-Félix Patassé utasafirishwa kutoka nchini Cameroun hadi Afrika ya kati alhamisi Mai 21 mwaka 2011.Rais huyo wa zamani wa nchini Afrika ya kati alifariki april 5 iliopita katika hospitaliya mjini Douala akiwa na umri wa miaka 74. rais huyo alilazwa katika haospitali hiyo baada ya kushindwa kuwasili nchini Guinea Equata. Mazishi yake yaibua tafrani nchini Afrika ya kati.

Matangazo ya kibiashara

Mwili wa hayati Ange-Félix Patassé utasafirishwa kutoka nchini Cameroun Mai 19 kwana 2011 na kupelekwa usiku hadi kaskazini mwa Afrika ya kati kwa kusubiri mazishi ya kitaifa yaliopangwa kufanyika Mai 21.

Kutokana na hali hiyo rais wa sasa wa Afrika ya kati François Bozizé ametangaza musba wa siku saba kuanzia jana siku ya jumapili hadi jumamosi Mai 2. Katika kipindi hicho bendera ya Afrika ya kati itasali nusu mlingoti nchi nzima na maeneo yote ulimwenguni kunako patikana uwakilishi wa nchi hiyo.

Mazishi ya rais huyo wa zamani yamezua tafrani. Wafuasi wake wanapinga kuhudhuria kwa wawakilishi wa serikali katika shughuli za mazishi za familia zilizopangwa kufanyika Mai 20 siku moja kabla ya mazishi yake.” Hatukubadilika katika msima wetu, amethibitisha hayo msemaji wa chama cha MLPC Guy Simplice Kodégué. Ni wafuasi pekee wa rais ndio wataoongoza shughuli za familia na hatutaki viongozi washiriki katika shguhuli za maadalizi ya mazishi za familia.”