Rwanda, Arusha

Ma jenerali wa Tano wakutwa na hatia

Jenerali Augustin Bizimungu mwaka 2003.
Jenerali Augustin Bizimungu mwaka 2003. photo : domaine public

Mahakama ya uhalifu wa kivita uliofanyika nchini Rwanda TPIR imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela  Augustin Bizimungu aliekuwa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo wakati yalipotokea mauaji ya kimbari nchini Rwanda kwa kuhusika moja kwa moja katika uhalifu huo

Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo iliokatwa jumanne hii kwenye makao makuu ya mahakama hiyo ya kimataifa TPIR mjini Arusha Tanzania imewahukumu vviongozi 4 wa jeshi la Rwanda zama za mauaji ya kimbari yaliotokea mwaka 1994. Miongoni mwa makamanda hao ni mkuu zamani wa majeshi na mkuu zamani wa polisi.

Mahakama hiyo imewakuta na makosa ya kuhusika moja kwa moja katika mauaji hayo baada ya kushindwa kuzuia mauaji dhidi ya watutsi na wahutu wenye msimamo wa wastani.

Meja François-Xavier Nzuwonemeye na capitaine Innocent Segahutu wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kuhuska katika kifo cha aliekuwa waziri mkuu zama hizo bi Agathe Uwilingiyimana pamoja na askari jeshi 10 wa Umoja wa mataifa waliokuwa wakimlinda katika usiku wa April 6 kuamkia April 7 mwaka 2004. Mawakili wa wanajeshi hao wameonyesha nia ya kukata rufaa.

Ama kuhusu viongozi hao zamani wa jeshi na wa polisi, mahakama ya TPIR imeachanisha kesi hiyo kwa kumkatia kifungo cha miaka 30 jela Jenerali Bizimungu na kuamuru aachiwe huru mkuu wa polisi jénéral Ndindiliyimana ambae tayari ametumikia kifungo. jaji wa mahakama Joseph Asoka de Silva amesema jenerali huyo alikuwa na uwezo mdogo wa kuzuia mauaji, na alikuwa akipendekeza mjadala baina ya wanyarwanda kabla ya kutokea mauaji hayo mwaka 1994. Jenerali huyo amedhihirisha furaha yake ya kuachwa huru baada ya kuzuiliwa katika kipindi cha miaka 11.

Takriban Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani walifariki dunia katika mauaji hayo ya kimbari yaliyochukua siku 100.

Bizimungu na Ndindiliyimana ni miongoni mwa viongozi waandamizi waliohukumiwa kwenye mahakama hiyo ya TPIR, iliyoundwa kusikiliza kesi za watu waliofanya uhalifu wakati wa mauaji hayo.