Libya

NATO yashambulia maeneo kadhaa mjini Tripoli

Moussa Ibrahim akitolea mwito NATO kusitisha mashambulizi na kuanzisha mazungumzo ya kuutanzua mzozo wa kisiasa nchini libya
Moussa Ibrahim akitolea mwito NATO kusitisha mashambulizi na kuanzisha mazungumzo ya kuutanzua mzozo wa kisiasa nchini libya REUTERS/Louafi Larbi

Ndege za kijeshi za Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi NATO zimefanya mashambulizi katika majengo ya idara ya Usalama na ya Ufisadi mapema leo asubuhi mjini Tripoli nchini Libya.

Matangazo ya kibiashara

Majengo hayo yanapakana na makaazi ya rais wa nchi hiyo kanali Mouamar Gadaffi. Shambulizi hilo limewajeruhi wafanyakazi kadhaa waliokuwa kazini.

Serikali ya Libya kupitia msemaji wake Mussa Ibrahim, imekashifu mashambulizi hayo na kuitaka NATO kusitisha mashambulizi mara moja.

MUSA IBRAHIM SP

Mashambulizi hayo yametokea siku moja baada ya kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kivita ya uhalifu ya ICC Louis Moreno Ocampo kutoa ombi kwa majaji wa ICC kutoa agizo la kukamatwa kwa kiongozi wa libya Mouamar Gadaffi na mwanae Seif Al islam na mkuu wa idara ya ujasusi kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji nchini humo.