Rwanda, Arusha

Serikali ya Rwanda yasema kuridhishwa na hukumu ya mahakama ya TPIR

Ramani Rwanda.
Ramani Rwanda. RFI

Serikali ya Rwanda inasema imeridhika na kufurahishwa na uamuzi wa mahakama ya kimataifa ya Arusha-TPIR, kumhukumu kiongozi wa zamani wa jeshi nchini humo Augustin Bizimungu miaka thelathini jela kwa kuhusika na mauaji ya kimbari nchini humo mwaka wa 1994.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama hiyo iliwakatia kifungo cha miaka 30 jela, mkuu zamani wa majeshi, na miaka 20 ya kifungo jela. Majenerali wengine waandamizi nao walihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja.

Bizimungu na Ndindiliyimana ni miongoni mwa viongozi waandamizi waliohukumiwa kwenye mahakama hiyo ya TPIR, iliyoundwa kusikiliza kesi za watu waliofanya uhalifu wakati wa mauaji hayo.

Hata hivyo, Ndindiliyimana, inasemwa alikuwa na "udhibiti mdogo" juu ya majeshi yake na alielezwa kupinga mauaji.

Kiongozi wa mashtaka wa Rwanda, Martin Ngoga amemwambia mwandishi wetu wa Kigali, Julian Rubavu kuwa haki imefanyika, ingawaje hawajaridhishwa na kifungo cha miaka 30.

MARTIN NGONGA 18