Afrika Kusini

Uchaguzi wa serikali za mitaa waanza leo nchini Afrika Kusini

Reuters/Siphiwe Sibeko

Wananchi nchini Afrika Kusini wanashiriki katika zoezi la kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa nchini humo, huku wananchi wakitumia kuwa uchaguzi huu utasaidia kuimarisha huduma nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Chama tawala cha ANC ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kikiongoza zaidi ya mikoa tisa nchini humo, kinakabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya chama cha upinzani Democratic Aliance ambacho kimeonyesha udhibiti wa Magharibi mwa taifa hilo.
Hapo juzi aliyekuwa rais Nelson Mandela aliendesha zoezi hilo la upigaji kura siku mbili kabla, kama wengine ambao hawawezi kufika kwenye vituo vya kupiga kura.
Wakfu wake ulitoa picha zake kwa mara ya kwanza za shujaa huyo mwenye umri wa miaka 92 aliyepambana na ubaguzi wa rangi tangu alipokuwa amelazwa hospitalini mwezi Januari.
Alifuatana na mkewe, mtoto wake wa kike na mjukuu wake.
Hakuwahi kutokea hadharani tangu sherehe za kumalizika kwa Kombe la dunia Julai 2010.
Waandishi walisema anazidi kuonekana dhaifu mara chache anazoonekana tangu kujiuzulu kuonekana hadharani mwaka 2004.