KENYA

Mahakama yasitisha Mazishi ya Wanjiru

Reuters/David Gray

Mahakama nchini Kenya alhamisi ya tarehe 18 May mwaka huu ilisitisha mipango ya mazishi ya aliyekuwa bingwa wa mbio ndefu Sammy Wanjiru mpaka uchunguzi wa namna kifo chake kilivyotokea utakapokamilika.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo ya mahakama imekuja baada ya mama mzazi wa Sammy,Ann Wanjiru kuiomba mahakama kutoa kibali cha kusitisha mazishi hayo kwa madai kuwa kuna mambo mengi yasiyo ya kawaida yanayoelezwa kuhusu kifo cha mwanae.

Uchunguzi wa mwili wa marehemu Wanjiru unatarajiwa kufanywa jumatatu ijayo .

Jopo la uchunguzi linaloongozwa na mkuu wa uchunguzi wa makosa ya jinai katika eneo la Nyandarua Charles Onyango unaendelea kupitia matukio yaliyorekodiwa na kamera za ulinzi siku moja kabla ya kifo cha mwanariadha huyo.

Marehemu Wanjiru alifariki dunia jumapili iliyopita baada ya kuanguka kutoka katika Roshani baada ya kutokea mtafaruku baina yake na mkewe.