Sudani-kusini

Waziri wa mafuta wa Sudani kusini ajiuzulu juu ya Abyei

Majumba yalioteketezwa kwa moto mjini Abyei Mei 23, 2011
Majumba yalioteketezwa kwa moto mjini Abyei Mei 23, 2011 Reuters

Waziri wa  kusini mwa Sudan katika serikali ya taifa amejiuzulu, amechukuwa uamuzi wa kujiuzulu na kusema kuwa uhalifu wa kivita umefanyika katika eneo lenye mzozo la Abyei. Luka Biong Deng hawezi tena kushirikiana na wenzake wa Sudan Kasakazini kutokana na uvamizi uliotokea katioka eneo hilo hivi karibuni. 

Matangazo ya kibiashara

Ni afisa mwandamizi kwenye chama tawala cha kusini, kinachotarajiwa kuiongoza Sudan kusini kwenye uhuru wake mwezi Julai.

Wakati huo huo, Baraza la umoja wa mataifa kitengo cha kutetea haki za binadamu, kimeshutumu majeshi ya Kahrtum kuvamia eneo la Abyei lenye utajiri mkubwa wa mafuta na kusababisha zaidi ya watu elfu kumi kutoroka makwao.

Wakati rais wa Sudan Kusini Salva Kir akikutana na wajumbe kutoka umoja wa mataifa huko Juba, rais wa Sudan Kaskazini Omar Al-Bashir amesema kuwa swala la Abyei litapata suluhu la kudumu,j ambo ambalo wachambuzi wa mambo wanasema kuwa haitawezekana kwa sasa na kinachostahili kufanyika ni kwa Sudan Kusini kujitangazia uhuru wake haraka iwezekanavyo kili kupata msaada kutoka kwa mataifa mengine na jamii ya kimatifa