Misri

Wanaharakati 3 wakamatwa nchini Misri, washukiwa kuandaa maandamano

Maandamano ya wananchi wa Misri mjini Cairo
Maandamano ya wananchi wa Misri mjini Cairo Reuters/Mohamed Abd El-Ghany

Mamlaka nchini Misri imewakamata wanaharakati watatu wakiwatuhumu kuhusika kuchochea maandamano ambayo yanatarajiwa kufanyika kesho siku ya Ijumaa,  kitu ambacho kimekatazwa na serikali.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa wanaharakati hao,  watatu ni pamoja na Muongozaji wa Filamu Aida Al Kashef aliyekematwa katika Jiji la Cairo ikielezwa alikuwa kwenye harakati za maandalizi ya maandamano hayo.

Wanaharakati hao wanarifiwa kuandaa mapinduzi mengine baada ya kufaanikiwa kuuangusha utawala wa Rais Hosni Mubaraka mapema mwezi January ambapo wanachi walishikiri baada ya kuchoshwa na uongozi wake.