Libya, Afrika Kusini

Zuma aelekea nchini Libya kumshawishi Gadaffi kuondoka madarakani

Gadaffi na Jacob Zuma, Trípoli, April 10, 2011.
Gadaffi na Jacob Zuma, Trípoli, April 10, 2011. ®Reuters

Wakati NATO ikizidisha mashambulizi nchini Libya, huku waasi wa kisherehekea siku 100 tangu kuanzishwa kwake, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anataraji kuzuru Tripoli Jumatatu hii, Mei 30, 2011. Rais Zuma atakutana na Kanali Muammar Gaddafi kama mwanachama wa Jopo la Umoja wa Afrika na kumpa maependekezo ya jinsi gani ya kuodoka madarakani. 

Matangazo ya kibiashara

Duru kutoka ikulu ya rais wa afrika kusini zaarifu kuwa serikali ya nchi hiyo imekuwa ikijadiliana na ile ya Uturuki kutafuta mkakati wa jinsi gani Mouammar Gadaffi aweza kuondoka. Jacob Zuma anatakiwa kumshawishi jamaa yake wa tangu muda mrefu kuondoka madarakani.

Hata hivyo kwenye agenda ilioandaliwa na Umoja wa Afrika ambayo inatakiwa kuwekwa mezani na rais wa Afrika kusini katika majadiliano swala hilo la kuondoka kwa Gadaffi halikuwekwa. Lakini wiki iliopita nchi za Senegal na Gambia zimekuwa nchi za kewanza barani Afrika kuutambua utawala wa Uasi wa CNT kama utawala halali nchini Libya.

Nchi zingine barani Afrika zaweza pia kufuata msimamo huo, hasa kubadili msimao kwa Rusia kwaweza pia kuleta mabadiliko iwapo Jacob Zuma atapendekeza kwa kiongozi huyo kuondoka kwa madarakani kwa heshma.

Upande mswingine, viongozi hao wawili watajadili kuhusu swala laAnton Hammerl mpiga picha raia wa Afrika kusini alieuawa mwezi April nchini lIBYA. Familia ya hayati huyo ilimuomba rais Zuma asaidie katika shughuli za kuusafirisha mwili wa hayati huyo hadi nchini Afrika Kusini. Jacob Zuma aliahidi kufanya kilka awezalo ili kuutafuta mwili wa mpiga picha huyo raia wa Afrika Kusini