Nato yashambulia tena, wakati Gaddafi akidai kuwa yu tayari kumaliza machafuko Libya
Imechapishwa: Imehaririwa:
Mpatanishi Mkuu kwenye mgogoro wa Libya Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema Kiongozi wa taifa hilo Kanali Muammar Gaddafi yupo tayari kutekeleza maagizo ya Umoja wa Afrika ya kumaliza mapigano kati ya majeshi yake na Waasi.
Rais Zuma amesema matumaini yapo na sharti la kwanza ni mashambulizi ya Majeshi ya NATO yakomeshwe lakini hakuna maelezo ambayo yanaanisha kama Kanali Gaddafi yupo tayari kuondoka madarakani.
Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa kauli ya Kanali Gaddafi ni ya kutia matumaini lakini wanahisi kuna umuhimu wa yeye kukutana na waasi ili kumaliza mtafaruku kama anavyoeleza Brian Wanyama kutoka Chuo Cha Masinde Muniro nchini Kenya.
Gaddafi ametawala taifa hilo kwa zaidi ya miongo minne sasa.