Libya, Italia

Waziri wa mambo ya nje wa Italia azuru ngome ya waasi mjini Benghazi

Italia imeendelea kusisitiza kuwa iko tayari kushirikiana na baraza la taifa la mpito nchini Libya ili kuimarisha mahusiano yao ya kiuchumi na kisiasa. hayo ni wakati waziri wa mambo ya nchi za nje wa Italia Franco Fratini akizuru mjini Benghazi makao makuu ya waasi wa Libya.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Italia Franco Fratini amewaambia waandishi wa habari wakati wa mkutano wake na waziri wa mambo ya nje upande wa waasi Ali al-Essawi kuwa utawala wa Ghaddafi umefikia kikomo na kwamba anatakiwa kuachia ngazi na kuondoka nchini Humo.

Hayo yanajiri wakati ripoti kutoka kwa mjumbe wa Umoja wa Afrika ,rais Jackob Zuma wa Afrika kusini aliyekutana na Ghaddafi hapo jana ikieleza kuwa kiongozi huo hana mpango wa kuondoka Libya ingawa yuko tayari kufanya mazungumzo na waasi ili kumaliza mapigano.