Sudani-Ethiopia

Ethiopia yajitolea vikosi vyake nchini Sudani

Nyumba zikiteketezwa kwa moto mjini  d'Abyei, Mei 23, 2011.
Nyumba zikiteketezwa kwa moto mjini d'Abyei, Mei 23, 2011. Reuters

Serikali ya Ethioipia inasema itatuma majeshi yake, katika eneo la Abyei kuweka amani ikiwa Sudan Kusini na Kaskazini itakubali hilo, wakati pande hizo mbili zikisaka suluhu la kudumu kuhusu ni nani halisi mmiliki wa eneo hilo. 

Matangazo ya kibiashara

Sudan Kusini imekubali wito wa Ethiopia wakati sudan Kaskazini, ikisema kuwa inafikiria, na wachambuzi wa maswala ya Sudan wanasema kuwa hatua hiyo ya Ethiopia ni nzuri na Umoja wa Afrika unastahili kuiga hatua hiyo.

Takriban watu milioni moja na nusu walikufa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya kaskazini na kusini vilivyodumu kwa miaka 22 na kumalizika mwaka 2005.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililaani udhibiti wa Abiyei na kutoa wito wa kuondolewa kwa haraka kwa wanajeshi wa kaskazini katika eneo hilo lenye utajiri wa mafuta ambalo upande wa kusini pia unadai ni lake.