Côte d'Ivoire

Serikali yatangazwa nchini Côte d'Ivoire

Guillaume Soro, waziri mkuu nchini Cote d'Ivoire
Guillaume Soro, waziri mkuu nchini Cote d'Ivoire AFP/Sia Kambou

Baraza la mawaziri la serikali ya Rais Alassane Dramane Ouattara yatangazwa jana jumatano Mosi Juni, 2011. Jambo la kwanza la kutambuwa katika serikali hiyo hamna mjumbe hata mmoja wa serikali ya Laurent Gbagbo. Baraza hilo lenye wajumbe 36 laongozwa na Guillaume Kibafuri Soro Wizara 14 ni kutoka chama cha rais Ouattara cha RDR, wizara 8 ni kutoka chama cha PDCI cha mshirika wake Henri Konan Bédié. Upande wa waasi zamani wa FN wamepewa wizara 5 akiwemo waziri mkuu Guillaume Kibafuri Soro huku wizara 5 zikipewa mashirika ya kiraia.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha RDR cha rais Ouattara ndichi chenye wizara nyingi, 14 dhidi ya 36 wanaongozwa na waziri mkuu Guillaume Soro. Chama cha PDCI cha Henri Konan Bédié mshirika wa karibu wa rais Ouattara nacho kimepewa wizara 8, FN waasi zamani hawa wamepewa wizara 5 wizara zilizo salia zimepewa mashirika ya kiraia na vyama vilivyo jiunga katika muungano wa RHDP.

Serikali hiyo inao mawaziri wa taifa 5 ambao ni watu wa karibu sana na rais Ouattara bila kujali vyama wanavyotokea, mathalan waziri wa mambo ya ndani Hamed Bakayoko ni mmoja kati ya watu wa karibu sana na raia, waziri wa ammbo ya ndani Daniel Kablan Duncan ambae aliwahi kuwa waziri mkuu katika utawala wa Henri Konan Bedie mwanachama wa PDCI, lakini Allasane Ouattara anafurahiya utendaji wake kazi baada ya kutumika nae miaka ya nyuma.

Wizara ya Fedha na Uchumi imepewa bila mshtuko Charles Diby Koffy mtaalamu wa maswal aya uchumi anaeheshimika sana katika mzunguuko wa wanafedha. Uundwaji wa serikali hiyo umezingatia uwakilishi wa mikoa na eneo zote zinazo unda nchi hiyo ya Côte d'Ivoire.

Chama cha FPI cha rais wa zamani Laurent Gbagbo hakikuwakilishwa ambapo haikuwa mshtuko kwakuwa ilijulikana mapema kutokana ya chama hicho kutowa masharti ya kuachiwa huru kwa wanasiasa wake kabla ya kushiriki katika serikali hiyo. Ifahamike kuwa serikali hiyo itakuwa na muda maalumu kwani, baada ya uchaguzi wa bunge unaotarajiwa mwishoni mwa mwaka huu, itaundwa serikali nyingine mpya ambapo waziri mkuu mpya atatangazwa.