Ujerumani yawakubali waasi wa libya wakati mapambano yakipamba moto

Reuters/Andrew Winning

Serikali ya Ujerumani nayo imejiunga katika kundi la nchi ambazo zinawatambua waasi nchini Libya ikiwa ni moja ya hatua ya kuwaongezea nguvu katika mkakati wao wa kuiangusha serikali ya Kanali Muammara Gaddafi.

Matangazo ya kibiashara

Ujerumani inatamka kuwatambua waasi wakati huu ambapo mapigano makali yanaendelea kushika kasi katika maeneo ya Dafnia, Yafran na kwenye milima ya Berber ambapo waasi wanaelezwa kushambulia vibaya.

Nchi za Australia, Uingereza, Ufaransa, Gambia, Italia, Jordan, Malta, Qatar, Senegal na Marekani ni miongoni mwa nchi ambazo zinawatambua waasi kitu ambacho kimekuwa kikilaaniwa na serikali ambayo inasema nchi hizo ni wezi kama anavyoeleza Msemaji wa Serikali Moussa Ibrahim.