Uganda-DRC

Ubakaji bado ni tatizo sugu barani Afrika hususan Afrika Mashariki

Vitendo vya ubakaji barani afrika bado ni swala tete
Vitendo vya ubakaji barani afrika bado ni swala tete Reuters

Vitendo vya ubakaji bado ni tatizo katika nchi za Afrika na hususan Afrika Mashariki, changamoto inayowaathiri sana watoto na wanawake.

Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano yetu ya leo, mwandishi wetu wa jijini Kampala Tonny Singoro, amefuatilia kwa karibu adha wanayoipata wakimbizi waliokimbia machafuko huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na hapa anamhoji mwanamke mmoja ambaye si vema kutaja jina lake.

Mama huyu aliyeko katika hali mbaya, anaeleza jinsi alivyobakwa na watoto wake kuuwawa, sababu zilizomsukuma kuomba hifadhi nchini Uganda.