Sudani

El Bashir wa Sudani kuhutubia sherehe za kutangazwa rasmi taifa la Sudani Kusini

Maafisa nchini Sudan wamesema, Rais wa nchi hiyo, Omar Hassan al Bashir atahutubia katika sherehe za uhuru wa Sudan kusini mwishoni mwa wiki hii.

The Istambulian.blogspot.com
Matangazo ya kibiashara

Bashir aliunga mkono kura ya maoni iliyopigwa mwezi Januari iliyofungua milango kwa sudan kusini kuamua kujitenga na kaskazini,hatua ambayo itakamilishwa siku ya jumamosi tarehe 9.

Serikali ya sudani kusini imesema hii leo kuwa viongozi wa takriban nchi 30 za Afrika wanatarajiwa kushiriki katika shamrashamra hizo sambamba na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki Moon na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza william Hague.

Hata hivyo kumekuwa na hali ya wasiwasi wa kutokea machafuko katika mpaka wa kordofan kusini na mji wenye mgogoro Abyei.