Mfumo wa usafiri wa gesi kuotka Misri kuelekea Israle na Jordan waharibiwa na bomu
Imechapishwa:
Bomba linalopitisha gesiĀ mjini Sinai limelipuliwa kwa Bomu na kusababisha moshi mzito kutanda angani halikadhalika kuharibu mfumo wa usafirishaji wa gesi kuelekea Israel na Jordan.
Maafisa usalama wamesema kabla ya tukio gari moja lilikuwa limeegeshwa karibu na bomba hilo katika eneo la Bir al -Abd muda mfupi kabla ya kutokea kwa mlipuko.
Maafisa waJordan wanaotegemea kwa kiasi kikubwa gesi ya kutoka Misri, wamekuwa na mazungumzo na maafisa nchini Misri kutathimini madhara na kutafuta mwafaka wa tatizo hilo.
Tukio hilo ni la tatu kutokea eneo hilo tangu mwezi februari wakati wa machafuko ya kumuondosha aliyekuwa rais wa Misri,Hosni Mubarak