Uturuki-Libya

Uturuki yavunja uhusinao na Tripoli

Reuters

Uturuki imetangaza Julay 3, 2011 kuvunja uhusiano wake na serikali ya libya na kumrejesha nyumbani balozi wake aliekuwa mjini Tripoli na kuweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Kiongozi wa Libya Kanali Muamar Gaddafi. Serikali ya Uturuki imetangaza kuwatambuwa waaasi wa Libya kama wawakilishi halali wa Libya.

Matangazo ya kibiashara

Katika ziara yake aliyoifanya katika mji wa Benghazi ulio ngome ya waasi, Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amesema baraza hilo ni wawakilishi halali wa watu wa Libya.

Wakati huohuo waasi wa Libya wameonesha matumaini yao juu ya mustakabali wa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi. Waziri wa zamani wa sheria na kiongozi wa waasi Mustafa Abdel Jalil amesema Gaddafi anaweza akabakia katika nchi hiyo, iwapo atakubali kujiuzulu. Lakini hata hivyo mmoja ya wasaidi wa kiongozi huyo wa waasi amepinga kuwepo uwezekano huo.