Libya, Benghazi

Waasi wa Libya watofautiana kuhusu hatma ya Gaddafi

Mkuu wa Baraza la waasi nchini Libya, Mustafa Abdel Jalil amesema hakuna uwezekano wa kiongozi wa Libya, Muamar Gaddafi kubaki nchini Libya na kuongeza kuwa lazima aondolewe madarakani na kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.

Mustafa Abdel Jalil, mkuu wa baraza kuu la waasi nchini Libya
Mustafa Abdel Jalil, mkuu wa baraza kuu la waasi nchini Libya REUTERS/Mohammed Salem
Matangazo ya kibiashara

Ghadhabu iliwakumba raia wa Libya hapo jana baada ya kupata taarifa kuwa baraza la waasi limeruhusu Gaddafi kubaki nchini Libya

Takriban watu mia moja walikusanyika nje ya jengo la hoteli ambayo mkuu wa baraza hilo alikuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari.

Wakati wanachama wa baraza la waasi wakisisitiza kuondoka madarakani kwa gaddafi, hakuna makubaliano ya pamoja juu ya kufanya mazungumzo ama la ili kumpa fursa Gaddafi kuondoka madarakani.

Hapo awali ilitolewa taarifa ya waasi kukubaliano na pendekezo la Gaddafi kubaki nchini Libya baada ya kuondolewa madarakani.