Nigeria-Maiduguri

Watu zaidi ya 10 wauawa, wengine zaidi ya 13 wamejeruhiwa mjini Maiduguri nchini Nigeria

Watu zaidi ya kumi wamedhibitishwa kufa na wengine 13 wamejeruhiwa kufuatia shambulio la bomu lililolenga soko moja la polisi katika mji wa Maiduguri nchini Nigeria.

(Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa vikosi vya jeshi la Nigeria vilivyosambazwa katika mji huo brigedia jenerali, Jack Okechukwu amedhibitisha kutokea kwa shambulio na kuongeza kuwa miongoni mwa watu watano waliokufa ni maofisa wa polisi.

Kiongozi huyo amesema kuwa shambulio hilo limetekelezwa wakati ambapo maofisa wa jeshi pamoja na familia zao walikuwa wakinunua mahitaji katika soko hilo kabla ya mtu mmoja kuwashambulia kwa risasi na baadae kulipua bomu na kuu watu 10.

Mji wa Maiduguri kwa majuma kadhaa sasa umekuwa katika hali ya sintofahamu kufuatia mashambulizi ya mfululizo yanatajwa kutekelezwa na kundi la kiislamu lenye msimamo mkali nchini humo la Boko Haramu.