Sudani

Mashambulizi mpakani Sudani siku chache kabla ya kutangazwa uhuru wa Sudani

Reuters/Tim McKulka/Unmis Handout

Majeshi ya Sudani yameanzisha mashambulizi ya anga zikiwa ni jitihada za kudhibiti maeneo yennye mafuta ikiwa ni wiki kadhaa kabla ya uhuru wa Sudani kusini. Msemaji wa majeshi ya sudani kusini SPLA ,Philip Aguer amethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi hayo yalifanywa na majeshi ya sudani kaskazini SAF dhidi ya viwanja vinavyowakutanisha wanajeshi wa SPLA .

Aguer amesema majeshi yake yako kwenye tahadhari kubwa kwa hivyo wanajiimarisha kwa kuwa wanahofia kuanza kwa matendo ya uvamizi ili kudhibiti maeneo yenye mafuta.