Sudani

Sudani kusini na Sudani kaskazini wakubaliana kuendeleza majadiliano ya kutatuwa mizozo mipakani

Ramani ya Sudani
Ramani ya Sudani @ RFI

Serikali za Sudan Kusini na Kaskazini siku ya jumatatu kwa mara nyingine zimekubaliana kuendelea na mazungumzo ya kutatua mgogoro katika mipaka ya nchi zao hata baada ya Sudani Kusini kutangazwa taifa huru siku ya Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo yametangazwa na viongozi wa nchi za pembe mwa Afrika wakati wa mkutano wa IGAD uliofanyika mjini Addis Ababa Ethiopia ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia mgogoro wa nchi ya Sudan.

Mkutano huo wa nchi wanachama Saba ulihudhuriwa pia na rais wa Sudan Kaskazini Omar Hassan al-Bashir na rais wa Sduna Kusini Salva Kiir ambao kwa pamoja walikubaliana kuendelea na mazungumzo ya kutatua mgogoro katika maeneo ya mipaka yao hata baada ya Sudan Kusini Kujitenga.

Viongozi hao wa IGAD mbali na kutangaza azma ya nchi hizo mbili pia wametoa wito kwa Umoja wa Afrika AU na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa UN kuchukua hatua dhidi ya nchi ya Eritrea ambayo wamedai imekuwa ikitumia biashara ya madini kufadhili vikundi vya mtanadao wa kigaidi kaskazini mwa Afrika.