Uganda

Mahakama ya Gulu nchini Uganga imeanza kusikiliza kesi ya wahalifu wa kivita

Joseph Kony, kiongozi wa  LRA,
Joseph Kony, kiongozi wa LRA, AFP

Mahakama mjini Gulu kaskazini mwa nchi ya Uganda kwa mara ya kwanza imeanza kusikiliza kesi za wahalifu wa kivita inayowahusisha viongozi wa juu wa kundi la Lord's Resistance Army.

Matangazo ya kibiashara

Kanali wa zamani wa juu wa wapiganaji wa LRA Kwoyelo Thomas ndie aliyekuwa wa kwanza kupandishwa kizimbani kujibu mahstaka 53 ya uhalifu wa kivita yanyimkabili ambapo amekana kuhusika na mashtaka yote dhidi yake.

Kundi la LRA linashutumiwa kufanya uhalifu wa kivita katika eneo la Gulu, ikiwemo vitendo vya ubakaji, utumikishaji wa watoto vitani, uharibifu wa mali na kufanya mateka raia wasio na hatia.

Tangu kuingia madarakani kwa rais Yoweri Museveni kwa mapinduzi ya mwaka 1986 kundi la LRA limekuwa likiendesha uasi wa vita vya msituni vikiongozwa na kiongozi wa kundi hilo Joseph Konny.

Zaidi ya watu milioni 1 na laki 8 walikosa makazi ya kuishi na maelfu kupoteza maisha kutokana na vita hivyo.