Nigeria

Mlipuko wa bomu wa wauwa watu 3 na kuwajeruhi wengine 9 mjini Suleija nchini Nigeria

Watu watatu wameuawa na wengine saba wamejeruhiwa kwa bomu lililolipuka jana katika eneo lililo karibu na kanisa la ALL CHRISTIAN FELLOWSHIP MISSION mjini Suleija nchini Nigeria.

Mlipuko nchini Nigeria
Mlipuko nchini Nigeria Reuters / Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Mchungaji wa kanisa hilo, Olowosagba amesema ibada ilikuwa imekwisha lakini baadhi ya waaumini walikuwa kanisani humo kabla ya kulipuka kwa bomu hilo.

Wakati huo huo jeshi la nchini humo limesema limeua watu kumi na mmoja wafuasi wa kikundi cha kiislam chenye msimamo mkali kinachoshutumiwa kuhusika na mfululizo wa mashambulizi ya mjini Maiduguri,kaskazini mwa Nigeria siku ya jumamosi usiku,huku raia wakilishutumu jeshi kuwashambulia kwa risasi.

Mfululizo wa ulipukaji wa mabomu na mashambulio mengine yalianza hasa baada ya uchaguzi wa wabunge,urais na viongozi wa majimbo uliofanyika mwezi wa Aprili na umekuwa ukiendelea kushika kasi wiki za hivi karibuni.