Zimbabwe

Polisi nchini Zimbabwe yawaachia huru wabunge wa upinzani baada ya kuwahoji

Baada ya kuwashikilia kwa saa kadhaa ikiwahoji, polisi nchini Zimbabwe imewaachilia huru wabunge watatu wa chama cha Movement for Democratic Change Incube kilichojitenga toka chama cha waziri mkuu Morgan Tshangirai.

Bendera ya Zimbabwe
Bendera ya Zimbabwe RFI
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa chama hicho Kurauone Chiwayi amesema amethibitisha kukamatwa na kuachiliwa huru kwa wabunge hao watatu bila ya kufunguliwa mashtaka yoyote na polisi.

Wabunge hao akiwemo rais wa Chama hicho Welshman Ncube ambaye na waziri wa biashara akiwa pamoja na viongozi wengine wa chama hicho walikamatwa katika mji wa Hwange mashariki mwa nchi hiyo siku ya jumapili na kuachiliwa usiku wa kuamkia jumatatu.

Chama hicho kimekua kikishutumu serikali ya Umoja wa kitaifa nchini humo chini ya rais Robert Mugabe na waziri mkuu Tsvangirai kwa kuvinyima uhuru vyama vidogo vya upinzani kufanya mikutano ya hadhara.