Senegal-Chad

Senegal yabadilisha uamuzi wake wa kumrejesha rais wa zamani wa Tchad nchini mwake

Rais wa zamani wa Tchad Hissène Habré, Novemba 2005 mjini Dakar
Rais wa zamani wa Tchad Hissène Habré, Novemba 2005 mjini Dakar AFP PHOTO SEYLLOU

Senagal imebadili maamuzi yake ya kumrudisha mtawala wa zamani wa Tchad Hissène Habré nchini mwake ambako anakabiliwa na adhabu ya kifo kwa makosa ya ukiukaji wa haki za binaadam.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imekuja kufuatia mkuu wa maswala ya haki za binaadam kutoka Umoja wa Mataifa, Navi Pillay kupinga uamuzi wa awali wa Senegal na kusema kuwa atakaporudishwa Chad atapata mateso na hatapata haki katika kesi inayomkabili.

Sheria ya kimataifa dhidi ya mateso inasema, Senegal haitamfukuza mtu kuelekea kwenye nchi ambayo inaaminika kuwa kumfukuza huko kutahatarisha usalama wake katika nchi husika.

Habre alitawala Tchad tangu mwaka 1982 mpaka 1990, alipoondolewa madarakani na Jenerali Idris Deby Itno na kukimbilia uhamishoni nchini Senegal.