Serikali ya Cameroon kutangaza hatuwa mpya za upigaji kura
Serikali ya Cameroon imetangaza utaratibu wa upigaji kura ambao utaruhusu hata raia wake wanaoishi nje ya nchi hiyo kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwezi wa kumi mwaka huu.
Imechapishwa:
Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Marafa Hamidou Yaya ametangaza uamuzi huo wa serikali ikiwa imebaki miezi michache kabla ya nchi hiyo haijafanya uchaguzi mkuu.
Uamuzi huo wa serikali pia umekuja baada ya vyama vya upinzani nchini humo kutishia kuharibu uchaguzi huo endapo rais Paul Biya na serikali yae wasingefanya marekebisho katika mapndekezo waliyoyatoa.
Wanasiasa na wanaharakati nchini humo wamekuwa wakishinikiza serikali yao kupitisha utaratibu huo wa kuruhusu raia wake walioko nje ya nchi kupiga kura kwa kile walichoeleza kuna zaidi ya raia milioni 5 wanaoishi mataifa mbalimbali duniani.
Rais Biya ameiongoza nchi ya Cameroon tangu mwaka 1982 ambapo hivi karibuni alibadili katiba ya nchi hiyo kumuwezesha kuwania kipindi kingine cha uraisi.