Waandamanji waendelea kukesha nchini Misri siku ya pili kititi
Waandamanaji nchini Misri wameendelea kukesha kwa usiku wa pili katika viwanja vya Tahriri mjini Cairo siku ya jumapili na kuapa kuwa kuendelea kukesha hapo bila kujali ahadi za waziri mkuu wa nchi hiyo,Essam Sharaf.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Wanaharakati walipiga kambi katika viwanja hivyo baada ya maandamano makubwa kufanyika siku ya ijumaa kushinikiza mabadiliko ya kisiasa.
Waandamanaji wameapa kuendelea kukaa kwenye viwanja hivyo mpaka madai yao yatakapotimizwa.
Waandamanaji wanadai kukoma kwa kesi za kijeshi dhidi ya raia,kufukuzwa kazi na kufunguliwa mashtaka kwa maafisa polisi waliokuwa wakisutumiwa kwa mauaji na unyanyasaji,kabla na baada ya mapinduzi na kuendeshwa kwa uwazi kwa kesi dhidi ya waliokuwa maafisa wa utawala wa Mubarak