Nigeria-Maiduguri

Bomu la mkononi lawauwa zaidi ya wanajeshi 2 kasakazini mwa Nigeria

Zaidi ya wanajeshi wawili wamejeruhiwa kaskazini mwa nchi ya Nigeria kufuatia shambulio la bomu la kutupwa kwa mkono lililoelekezwa kwenye gari la doria la mjini Maiduguri.

Mji wa Maiduguri makao makuu ya kundi la boko haramu
Mji wa Maiduguri makao makuu ya kundi la boko haramu RFI / Julie Vandal
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi katika mji huo Viktor Ebaleme amesema kuwa shambulio hilo limetekelezwa na watu wasiofahamika ambapo walilenga kulipua gari la jeshi lililokuwa doria katika eneo hilo bila ya mafanikio lakini lilijeruhi askari wawili.

Shambilio hilo ni mfululizo wa mashambulizi mengine yanayoshukiwa kufanywa na wapiganaji wa kundi la Boko Haram katika mji wa huo, amabpo siku ya jumanne walifanya shambulio kama hilo katika mji wa Bulunkutu.

Maelfu ya wananchi mjini maiduguri wameanza kuyakimbia makazi yao kuelekea miji jirani kufuatia hofu ya kuzuka kwa machafuko zaidi kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa Boko Haram.