Waziri mkuu wa Tunisia atowa mwito kwa vyama vya upinzani kurejea katika kamati ya majadiliano
Kufuatia kutangaza kujitoa kwa baadhi ya vyama vya upinzani nchini Tunisia kwenye kamati maalumu ya kupitia mapendekezo ya kufanya mabadiliko nchini humo, waziri mkuu Beji Essebsi ametoa wito kwa vyama hivyo kurejea tena katika kamati hiyo.
Imechapishwa:
Kauli ya waziri mkuu huyo imekuja kufuatia mwezi mmoja uliopita chama cha Tunisia Islamist Movement na kile cha Congress for the republic kutangaza kujitoa katika kamati hiyo ya kitaifa ya kupitiasha mapendekezo ya kufanyika mabadiliko ya kidemokrasia nchini humo.
Kamati hiyo maalumu iliundwa mwezi wa pili mwaka huu baada ya kuangushwa kwa utawala wa Ben Ali ambapo lengo lake ilikuwa ni kupitia na kupitisha mabadiliko ya mfumo wa serikali na demokrasia.
Kamati hiyo imejumuisha wawakilishi wa vyama vya siasa, asasi za kiraia, vyama vya wafanyakazi na wanasheria.