Sao Tome

Changamoto kadhaa zajitokeza saa chache kabla ya kampeni za Urais kuhitimishwa nchini Sao Tome

Ramani ya Sao Tome
Ramani ya Sao Tome France diplomatie

Ikiwa zimesalia saa chache kabla ya kuhitimishwa kwa kampeni za urais katika visiwa vya Sao Tome vilivyoko kaskazini magharibi mwa Afrika tayari changamto mbalimbali zinazowakabili wagombea wa kinyang'anyiro hicho zimeanza kubainishwa.

Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo ambayo inakabiliwa na hali mbaya ya uchumi, umasiki pamoja na rushwa inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu siku ya jumapili, uchaguzi ambao unatarajiwa kuwa wenye mvutano kutokana na upinzani kupewa nafasi kubwa ya kutwaa kiti hicho.

Wagombea kumi wanatarajiwa kuchuana katika uchaguzi huo kurithi nafasi ya rais wa sasa Fradique de Menezes, huku wachambuzi wa mambo wakimpa nafasi mgombewa upinzani Manuel Pinto da Costa kushinda uchaguzi huo.

Ripoti ya hivi karibuni ya umoja wa mataifa imeonyesha kuwa nchi hiyo inakabiliwa na baa la umasikini ambapo zaidi ya wananchi laki mbili wanaishi katika hali duni.