Senegal-Dakar

Rais wa Senegal avunja ukimya kwa mara ya kwanza tangu kuzuka maandamano nchini mwake

Rais wa Senegal Abdoulaye Wade.
Rais wa Senegal Abdoulaye Wade. Reuters/Finbarr O'Reilly

Rais wa Senegal Abdulaye Wade, amevunja ukimya kwa mara ya kwanza hapo jana tangu kuzuka kwa maandamano katika taifa hilo hilo mwezi uliopita na kuweka wazi kuwa anatarajia kuwania tena nafasi ya urais hatua iliyoleta changamoto kubwa kwa wanaomtaka kuondoka madarakani.

Matangazo ya kibiashara

Wade amesema yu tayari kufanya uchaguzi ndani ya siku 40 mpaka 60 badala ya kusubiri mpaka mwezi Februari mwaka ujao wakati kipindi chake cha miaka mitano kitakapokuwa kimekwisha.

Maandamano yaliyoanza wiki ya mwisho ya mwezi june yalikuwa mabaya zaidi katika kipindi chake cha miaka kumi na mmoja madarakani na kupatia nguvu upinzani ya kumtaka aachie madaraka kama inavyoelezwa katika katiba ya nchi hiyo.