Malawi-Uingereza

Uingereza yatangaza kusitisha msaada kwa serikali ya Malawi

Serikali ya Uingereza imetangaza kusitisha msaada wa fedha kwa serikali ya Malawi kwa kile kinachoelezwa serikali ya nchi hiyo kushindwa kutilia mkazo maswala yahusuyo uchumi na uongozi.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya maendeleo ya kimataifa ya nchini uingereza imeishutumu serikali ya malawi kwa kuzuia maandamano, kuzitisha asasi za kiraia na utungaji wa sheria zinazokandamiza wanasiasa wa upinzani.

Katika taarifa yake, Katibu wa ofisi hiyo,Andrew Michel amesema watu wa malawi na raia walipa kodi wa uingereza wameangushwa na serikali ya malawi, kwa hivyo anasitisha msaada wa fedha kwa bajeti ya malawi.

Hata hivyo Mitchel ameahidi kutumia namna nyingine kuhakikisha kuwa raia wa malawi wanapata huduma bora za afya na elimu.