Guinea

Jeshi nchini Guinea laendelea kuwakamata washukiwa wa jaribio la mapinduzi nchini humo

Operesheni ya kamata kamata inaendelea huko Guinea baada ya jaribio la mapinduzi la Julay 19. Askari wengi wanaokamatwa ni wa karibu sana na rais wa utawala wa mpito Sekouba Konate. Shemeji wa mpinzani wa rais Alpha Conde wakati wa uchaguzi Cellou DaleIn Diallo amekamatwa leo asubuhi.

Reuters/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Watu wa karibu na jenerali Sekouba Konate wakanusha kuhusika na tukio hilo na wakihoji faida ya kutekeleza tukio hilo.

Hata hivyo miongoni mwa waliokamatwa wapo ma jenerali Sadiki Kamara maarufu Degaulle pamoja na Nounou Thiam ambae alikuwa mkuu wa majeshi ya nchi  wakati wa utawala wa mpito ambae aliondolewa uongozini na Alpha Konde ambao ni watu wa karibu na rais wa serikali ya mpito ya zamani jenerali sekuba konatee.

Kulingana na duru hiyo hawana faida yoyote ya kuendesha uhaini huo na kusema kuwa unaweza pia kuwa umepangwa na upande wa rais kwani hayo yalishawahi kutokea.

Ma kanali wengine 2 wa jeshi la nchi hiyo Moussa Bonda Bon Camara na Chérif Dyaby ambao wanasdikiwa kuwa watu wa karibu sana na Moussa Dadis Camara wametiwa nguvuni. Kiongozi wa mapinduzi zamani nchini Guinea akiwa uhamishoni huko nchini Burkina Faso  amekanusha kuwa na ushirikiano na wanajeshi hao na kusema kuwa amesikitishwa na tukio hilo ambalo ameliita la uhaini.