Senegal

Serikali ya Senegal yapiga marufuku maandamano yoyote

Ousmane Ngom waziri wa mambo yani wa Senegal
Ousmane Ngom waziri wa mambo yani wa Senegal politico

Kufuatia kuendelea kutanda kwa hali tete ya kidemokrasia nchini Senegal, waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, Ousmane Ngom ametangaza serikali kupiga marufuku maandamano yoyote yaliyopangwa kufanyika siku ya jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Akiongea na waandishi wa habari mjini Dakar, waziri huyo amesema kuwa kutokana na sababu za kiusalama na hali ya kisiasa ilivyo hivi sasa nchini humo serikali haitaruhusu maandamano yoyote kwakuwa yanaweza kuchochea machafuko zaidi nchini humo.

Maandamano ya siku ya Jumamosi yameandaliwa na wanaharakati, vyama vya upinzani na asasi zisizo za serikali kupinga hatua ya rais wa nchi hiyo Abdoulaye Wade kuwasilisha muswada wa marekebisho ya katiba bungeni yatakayompa nafasi nyingine ya kuwania urais kwa kipindi kingine.

Waandamanaji hao wamepanga kuzingira ofisi kadhaa za serikali ikiwemo wizara ya mambo ya ndani, tume ya taifa ya uchaguzi na ikulu ya rais wade kumshinikiza kutowania kipindi kingine cha urais.

wakati huohuo shirika la Amnesty International limeomba uchunguzi ufantyike dhidi ya matokea ya juini 23 nchini Senegal wakati wananchi walipoandamana mjini Senegal wakati viongozi wa nchi hiyo walipojaribu kugeuza katiba ya nchi hiyo.

Kulingana na shirika hilo, kulikuwa na vitendo vya unyanyasaji vilivyotekelezwa dhidi ya waandamanaji ambao walikuwa na haki ya kuandamana.