Burundi

Watu 9 wauawa kaskazini mwa Burundi

Watu tisa wamedhibitishwa kaskazini mashariki mwa Burundi kufuatia mapigano kati ya polisi na watu wasiofahamika ambao walivamia eneo la mkoa wa kaskazini mwa Burundi wa Cibitoke.

Kanali Gaspard Baratuza, msemaji wa jeshi la Burundi
Kanali Gaspard Baratuza, msemaji wa jeshi la Burundi Burunditransparence.org
Matangazo ya kibiashara

Gavana wa Mkoa huo, Anselme Nsabimana amesema kuwa tukio hilo lilitokea siku ya jumanne asubuhi lakini kundi hilo la watu wasiofahamika waliendelea na mashambulizi dhidi ya polisi hadi jumatano usiku ambapo walifika eneo la tukio na kupata miili ya watu sita wakiwemo polisi wawili.

Msemaji wa jeshi kanali Gaspard Baratuza, amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa polisi walifanikiwa kuwadhibiti wapiganaji wa kundi hilo ambapo hakuna taarifa rasmi kuwa kundi hilo ni la mrengo gani.

Hili linakuwa shambulio baya zaidi kuwahi kufanyika nchini humo tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo mwaka 2005.

Matukio kadhaa ya kuyumbishwa usalama yanaripotiwa mnamo siku zote hizi za nyuma tangu pale ulipomalizika uchaguzi wa bunge na rais uliokipa ushindi wa kishindo chama cha CNDD-FDD. Vyama vya upinzani vilipinga ushindi huo na kudai wizi wa kura ulifanyika.

vyama hivyo vya upinzani vilijiunga katika muungano unajumuisha vyama zaidi ya 10 na kuomba mjadala na serikali ya sasa ili kutatuwa matatizo yaliopo.

Serikali upande wake imekuwa ikitowa msimaloo wake kwamba haiwezi kuzungumza na chama chochote kuhusu maswala ya uchaguzi kwani kilipata ushindi, jhivyo kinauwezo wa kutumia ushindi huo kadri kitavyo.

Hali ikiendelea kuwa hivyo, uvumi umetanda kuanzishwa uasi. Dalili za uasi huo zimeanza kujionyesha baada ya matukio kadhaa, huku serikali ikikanusha kuwepo uasi bali makundi ya majambazi yanayo pora pesa na mali za wananchi.