Libya-Ufarana

Ufaransa yawapa waasi wa Libya pesa zilizokuwa zinashikiliwa kutoka serikali ya Gaddafi

Waasi wa Libya kwenye uwanja wa mapambano
Waasi wa Libya kwenye uwanja wa mapambano REUTERS/Esam Al-Fetori

Ufaransa imetengeza kuwapatia Waasi nchini Libya ambao wanapambana na Serikali ya Kanali Muammar Gaddafi dola milioni mia mbili hasimni na kenda ambazo zimepatikana kutokana na mali za serikali walizokuwa wanazishikilia. 

Matangazo ya kibiashara

Baraza la Taifa la Mpito nchini Libya limekabidhiwa fedha hizo ili ziweze kuwa msaada katika kuhakikisha wanafanikiwa kuung'oa utawala wa Kanali Gaddafi madarakani sambamba na kukunua mahitaji ya kibinadamu.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa inaeleza kuwa fedha hizo zote zimepetikana baada ya kukamatwa kwa mali na fedha za Utawala wa Kanali Gaddafi ambazo zilikuwa zinahifadhiwa huko.

Naye Balozi Mpya anayewakilisha Waasi nchini Ufaransa Mansur Saif Al Nasr baada ya kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje Alain Juppe amesema fedha hizo ni mali ya wananchi wa Libya.

Waasi wa Libya wamejiapiza kuhakikisha wanatumia fedha hizo vyema ikiwemo ni pamoja na kununua chakula na dawa ambazo zinahitajika kwa haraka mno kutokana na wengi wa wananchi kuwa kwenye hali mbaya.