Somalia

Ukame wazidi kuiumiza Somalia, hofu ya vifo zaidi yatanda

RFI

Ukame ambao umetanda nchini Somalia umesamba kwenye mikoa mingine mitatau na hivyo kuongeza hofu ya watu wengi zaidi kupoteza maisha kipindi hiki ambacho mashirika mbalimbali yanajitahidi kupeleka misaada.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa, UN umeeleza hali imezidi kuwa mbaya wakati huu ambapo wananchi wameanza kukimbilia kwenye Mji wa Mogadishu ili waweze kujipatia chakula cha msaada kinachosambazwa.

Viongozi mbalimbali wameanza kufanya ziara huko Somalia akiwemo Rais wa Uswiss Micheline Calmy-Rey ambaye ameitaka Jumuiya ya Kimataifa kufanya kila linalowezekana kuokoa maisha ya wananchi hao.

Katika kauli yake Rais wa Uswiss Micheline Calmy-Rey amesisitiza upatikanaji wa chakula kwa wahitaji wa Chakula huko nchini Somalia.

Hali ya ukame bado ni tishio kwa nchi za pembe ya Afrika na hata Afrika Mashariki na hivyo jitihada madhubuti zinahitajika ili kukabiliana na njaa inayotokana na ukame katika maeneo hayo.