Kenya

Wanasiasa nchini Kenya walaumiana kushindwa kushughulikia swala la ukame

Serikali ya Kenya pamoja na wanasiasa wa taifa hilo wameingia lawamani kutokana na kushindwa kushughulikia suala la ukame na njaa inayowakabili watu zaidi ya milioni tatu huku wananchi wakiwa wamechangisha milioni tano nukta tatu hadi sasa.

Matangazo ya kibiashara

Jukumu la kutafuta chakula limechukuliwa na wananchi badala ya serikali au wanasiasa ambao walitarajiwa kuwa mstari wa mbele hasa kipindi hiki ambacho Eneo la Pembe ya Afrika linapita kwenye kipindi kigumu.

Wananchi wameshikwa na hasira zaidi baada ya mwezi uliopita Msemaji wa Serikali Alfred Mutua kuwaambia wanahabari kuwa hakuna takwimu ya mtu kupoteza maisha kutokana na kukosa chakula.