Malawi-IMF

Sarafu ya malawi yashuka kwa asilimia 10, kutekeleza masharti ya IMF

fr.123rf.cpm

Benki kuu nchini Malawi imetangaza kushusha thamani ya fedha ya nchi hiyo kwa asilimia 10 ikiwa ni hatua ya awali ya kutekeleza masharti ya Shirika la fedha Duniani IMF kuipatia mkopo nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Akiongea mjini Lilongwe msemaji wa benki kuu ya malawi. Perks Ligoya amesema kuwa hatua hiyo inalenga kufufa uchumi wa taifa hilo ambapo pia ametangaza kufanya marekebisho katika thamani ya fedha za kigeni ambapo sasa dola imepanda toka kwacha 150 hadi 167.

kuyumba kwa uchumi wa Malawi kulitokana na nchi hiyo kusitisha uhusiano wa kibalozi na nchi ya Uingereza ambayo imekuwa ikichangia nusu ya bajeti ya nchi hiyo pamoja na shirika la fedha duniani IMF kutangaza kushindwa kuisadia nchi hiyo kutokana na kushindwa kupunguza deni la taifa.

Serikali ya rais Bingu wa Mutharika imekuwa katika wakati mgumu kwa majuma kadhaa kufuatia maandamano ya nchi nzima yaliyoshuhudia watu 19 wakipoteza maisha kupinga hali mbaya ya uchumi.