DRC-UCHAGUZI

Rais Joseph Kabila athibitishwa na chama chake kuwa mgombea wa urais

Afriqueredaction

Chama tawala nchini Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo cha PPRD, kimemchagua kiongozi wa taifa hilo Joseph Kabila Kabange kuwa mgombea wa nafasi ya Urais, uchaguzi utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu wa chama cha People's Party for Reconstruction and Democracy PPRD, Evariste Boshab ametaarifu kuwa Kabila amechaguliwa kuwa mgombea kuwakilisha chama hicho.

Hayo yameelezwa baada ya mkutano mkuu uliohudhuriwa na wafuasi takriban 3500 wa chama hicho kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, hata hivyo bado Joseph Kabila hajathibitisha ikiwa atagombea tena nafasi ya urais utakaofanyika tarehe 28 mwezi Novemba ama la.

Mbali na rais Joseph Kabila, wagombea wengine ambao tayari wamekwisha idhinishwa na vyama vyao kuwania kiti hicho cha urais, ni Ethiene Chisekedi wa Mulumba, Vital Kamerhe, Oscar Kashala Lukumuenda wa chama cha (UREC), Guillaume Ngefa, Michel Okongo, Raphael Katebe Katoto wa chama cha (UPDC), Dr Nicodème Tumba wa chama cha (RAPHA) Gaspard-Hubert Lonsi Koko wa chama cha RDPC, Augustin Mukamba, Francis Mboyo au Ursoel Mayambu