Liberia-Kura ya maoni

Walinda amani wa UN watawanyika nchini Liberia siku moja kabla ya kura ya maoni

Uchaguzi jijini Monrovia nchini Libéria Octoba 11. 2005.
Uchaguzi jijini Monrovia nchini Libéria Octoba 11. 2005. Chris Hondros/Getty Images

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa (UN), wametanda sehemu mbalimbali nchini Liberia, siku moja kabla ya kuanza kwa kura ya maamuzi ya katiba, zoezi linalosusiwa na chama kikuu cha upinzani, Congress for Democratic Change.

Matangazo ya kibiashara

Kura hiyo inatarajiwa kuwa kipimo cha demokrasia, kwa taifa la Liberia, linalojiandaa kuitisha uchaguzi mkuu wa pili, baada ya kukumbwa na vita.

Chama cha CDC, kinadai kuwa mapendekezo hayo ya katiba, yanalenga kukifaidisha chama tawala, hasaa kipengele cha kupunguza muda wa mgombea kuishi nchini humo, kutoka miaka kumi hadi mitano, kigezo kitakachowapa fursa watu wengi zaidi kugombea, na kusababisha upinzani ugawane kura.