Ethiopia-AU

Viongozi wa AU kukutana kesho nchini Ethiopia

Afreeque

Viongozi kutoka mataifa ya Afrika wanatarajiwa kukutana kesho nchini Ethiopia kujadili namna ambavyo wanaweza kuisaidia nchi ya Somali ambayo inakabiliwa na ukame uliosababisha njaa kwa zaidi ya watu milioni kumi na mbili.

Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika AU Jean Ping amesema viongozi hao watakutana na kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kupata msaada wa haraka kuwakoa watu wanaokabiliwa na njaa nchini Somalia.

Wafuatiliaji wa Mambo wanaona kuwa huu ni wakati muafaka kwa Viongozi hao kukutana na kujadili kile ambacho kinaendelea nchini Somalia na Libya na kwengineko barani Afrika.